SHEIKH SHAMIIM " HIVYO NDIVYO VIGEZO VYA WALII (sehemu ya 1)"
10. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema ya kwamba, “Mtume (S.A.W.) kasema, "
«لاَ طَلاَقَ إِلاَّ بَعْدَ نِكَاحٍ، وَلاَ ظِهَارَ إِلاَّ بَعْدَ نِكَاحٍ، وَلاَ عِتَاقَ إِلاَّ بَعْدَ مُلْكٍ، وَلاَ نِكَاحَ إِلاَّ بِوَلِيٍّ وَصَدَاقٍ وَبَيِّنَةٍ».
Maana yake, “Hapana talaka ila baada ya (kufunga) ndoa, wala dhihari[1] ila baada ya (kufunga) ndoa, wala kumpa uhuru mtumwa ila baada ya kummiliki, wala ndoa (haifungiki) ila kwa walii[2], na mahari, na mashahidi”.
511. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«الأَيِّمُ أَحَقُّ بِنَفْسِهَا مِنْ وَلِيِّهَا، وَالْبِكْرُ تُسْتَأْذَنُ فِي نَفْسِهَا، وَإِذْنُهَا صُمَاتُهَا».
Maana yake, “Mwanamke alieolewa kabla anayohaki zaidi katika nafsi yake kuliko walii wake, na mwanamke bikira anaulizwa, na idhini yake ni kunyamaza kwake”.
No comments