JE! KUSWALI NA VIATU NI SUNNA?
SWALI
Je kusali na viatu ni katika Sunna?
السؤال: هل الصلاة بالحذاء من السنة؟
📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖
📘JAWABU الجواب 📘
➡Muisilaamu anatakiwa akitaka kuingia katika sala anatakiwa kuiandaa nafsi yake, mwili wake, pahala pa kusalia, na vazi lake pia.
المسلم يؤمر إذا أراد الصلاة أن يهيئ نفسه، بدنه ، مكان صلاته، ولباسه أيضا.
➡Kuhusu kusali na viatu jambo hili halipewi hukmu kiwa ni Sunna ambayo wanatakiwa waisilaamu kuifanya.
أما عن الصلاة بالحذاء فإن هذا الامر لا يعطى حكم سنة يطلب الناس بفعلها.
➡Hii inaingia katika hukmu ya kuwa inajuzu kusali na viatu , lakini kujuzu huko kuna patikana katika hali kama zifuatazo:
هذا يدخل في جملة جواز الصلاة بالحذاء، ولكن هذا الجواز يكون في الحالات كالتالية:
1- Ikiwa anasali pahala ambapo hawezi kusimama ila akiwa amevaa viatu: kama ardhi iliyo chemka kwa sababu ya jua, au sehemu yenye jangwa na mawe yenye ncha.
إذا كان أحد لا يستطيع أن يقوم للصلاة إلا وهو ينتعله؛ كما إذا أرض ساخنة، أو صحراء بانت أطراف الحجارة منها.
2- Akiwa ni katika safari na akashindwa kuvua viatu.
إذا كان على سفر ولا يتمكن من خلع الحذاء.
➡Amma akiwa katika hali ya kawaida basi hakuna ubora wala ruhusa ya kusali na viatu.
أما إذا كان في حالة عادية فليس ثم فضل ولا إذن في الصلاة بالحذاء.
➡Na hasa ukitazama hikma ya kusali na viatu katika zama hizi hakuna, kwa sababu misikiti yote iko katoka hali nzuri, na kuingia na viatu kuna haribu hali ya msikiti.
وخاصة إذا نظرت إلى الحكمة من الصلاة بالحذاء في عصرنا غير موجودة، وذلك لحسن حال المساجد، فالدخول بالحذاء فيه إفساد للمسجد.
➡Kisha viatu vilivyo ruhusiwa vina masharti yake maalumu , na miongoni mwayo ni:
ثم إن الحذاء الذي رخص بلبسه له شروط ومواصفات خاصة ، منها:
1- Viwe havina soli refu.
أن لا يكون متنه أو كعبه مرتفعا.
2- Viwe vimelingana vyote na awe sawa mwenye kuvivaa ikiwa atasimama.
أن يكون متساويا كلاهما بحيث يستقيم طولا من لبسهما.
3- Viwe wazi sehemu za mbele, ili vidole viguse ardhi wakati wa kusujudu.
أن يكون مفتوما من أمامه بحيث أصابع القدمين تمس الأرض في سجوده.
➡Naam
Mtume s.a.w aliswali siku hali ya kiwa amevaa viatu, kisha akaijiwa na Jibriil na kumuambia kuwa " Vua kiatu chako kwa sababu kimechukua najisi"
نعم؛
صلى رسول الله صلى الله عليه وسلم وهو منتعل، حتى جاءه جبريل عليه السلام وقال له: اخلع نعلك فإن بها قذاة - نجاسة"
➡Kwa hiyo hakuna ulazima wa kuvaa viatu katika sala, na ikiwa atavaa mtu viatu katika sala viatu vyenye sifa ambazo hazipelekei kuharibu sala, hatopata dhambi, japokuwa bora zaidi ni kuacha kufanya hivyo.
إذن ليس هناك لزوم لبس الحذاء في الصلاة، ومن صلى بالحذاء الذي استكمل تلك الصفات التي لا توجب فساد الصلاة، فإنه لا يأثم، وإن كان الأولى ترك التنعل.
➡ Mtume s.a.w hakuhimiza watu wavae viatu katika sala hata mara moja katika uhai wake.
النبي صلى رسول الله صلى الله عليه وسلم لم يحث الناس على لبس الحذاء في الصلاة مدى جياته.
➡Wala maswahaba r.a hawakuwa wakihimizana kusali na viatu katika misikiti.
ولا الصحابة رضوان الله عليهم ما كانوا يشجعون بعضهم بعضا على لبس الحذاء في الصلاة في المساجد.
➡Wala hakuna fadhila zozote zimetajwa katika kusali na viatu.
وليس هناك فضائل تذكر أو ذكرت عن لبس الحذاء في الصلاة.
➡Hii inaonyesha wazi kuwa jambo hili lilikuwa kwa mujibu wa hali tu inapo lazimu, na wala haikuwa ni jambo la lazima wala fadhila kulifanya.
وهذا يدل جليا على أن ذلك كان على مقتضى الحال في زمانهم، ولم يكن لازما ولا فضل في فعله.
➡Na dalili ya hayo pia ni katika uhalisia wa misikiti yote ukimwenguni, ambayo imeshikama na Qurani na Sunna, hawaruhusu kusali watu na viatu msikitini, wala kutufu navyo katika Al kaaba.
والدليل على ذلك أيضا واقع جميع المساجد في العالم، التي تتمسك بالقرآن والسنة، لا تسمح للناس بالصلاة في المساجد بأحذيتهم، ولا الطواف بها حول الكعبة.
➡Ni ajabu kuwepo baadhi ya watu wameshikilia jambo hili kwa nguvu kulifanya kana kwamba ni nguzo katika nguzo za sala, au sharti miongoni mwa masharti yake.
فيا عجبا ممن يتمسك بهذه المسألة ترخيصا في فعلها وكأنها ركن من أركان الصلاة ، أو شرط من شروطها.
➡Bali ukitazama hata katika Sheria ya Nabii Muusa a.s aliambiwa na Allaah sw:
" Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa."
حتى إذا نظرت في شريعة موسى عليه السلام، فقد أخبره الله تعالى كما في الآية :
(إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى)
[Surat Ta-Ha 12]
➡Namuomba Allaah sw atuongoze njia iliyo sawa.
أسأل الله تعالى أن يهدينا سواء السبيل
📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖
ALLAAHU AALAM الله أعلم
➡Jawabu kutoka kwa
U/ SHAABAN AL BATTAASHY.
📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖
No comments