Urusi inasema kuwa Rais Erdogan wa
Uturuki ameomba msamaha kwa hatua ya taifa lake, kuidungua ndege ya
kivita ya Urusi karibu na mpaka na Syria mwaka jana.
Katika ujumbe
ulioandikwa ndani ya barua hadi Kremlin kwa Rais Putin, Bwana Erdogan
alielezea masikitiko yake makubwa kwa kile kilichofanyika, huku akisema
anataka kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawiliUturuki bado haijatoa maelezo kuhusiana na barua hiyo.
Udunguaji wa ndege hiyo uliibua mgongano mkubwa wa kisiasa, uliopeleekea Urusi kuiwekea Uturuki vikwazo vya kibiashara ambavyo vingeondolewa tu baada ya Rais Erdogan kuomba msamaha.
No comments