Header Ads

Cup of coffee on saucer

FOMULA YA KWENDA PEPONI NI MOJA TUUU

Image result for paradise725- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: "Mwanamke akiswali Swalah zake tano, akafunga mwezi wake, akahifadhi tupu yake na akamtii mume wake, ana haki ya kuingia Peponi." Imepokelewa na al-Bazzaar kupitia kwa Anas, Ahmad kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan az-Zuhriy na at-Twabaraaniy kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Hasanah. as-Suuyuutwiy amesema ni Swahiyh. "Mwanamke akiswali Swalah zake tano... - Bi maana zile Swalah tano za kila siku, Swalah za faradhi. ... akafunga mwezi wake... - Bi maana Ramadhaan ikiwa hana hedhi. ... akahifadhi tupu yake na akamtii mume wake... - Bi maana kwa yale ambayo sio maasi. ... ana haki ya kuingia Peponi." - Bi maana ikiwa atajiepusha na madhambi makubwa, akatubu kikwelikweli au akasamehewa. Ina maana ataingia Peponi na wale watu wa kwanza watakaoingia. Hata hivyo Waislamu wote wataingia Peponi hata kama wataadhibiwa hapo mwanzo kwa kuingizwa Motoni. Ikiwa utauliza kwa nini imewekewa mpaka kwa Swalah na Swawm na si katika nguzo zingine za Kiislamu, hili ni kwa sababu wanawake wana mazowea ya kupuuzia Swalah na Swawm, ni wenye kuwaharibu na kutowatii waume. Vilevile wanawake huwa hawana pesa za Zakaah ya faradhi na Hajj. Kwa njia hiyo akataja hukumu hii kwa mafungamano na yanayojitokeza mara nyingi na kuwahamasisha kwa yale ambayo kila siku wanatakiwa kuyahifadhi na kuyadhibiti. Tupu inahusu tupu ya mbele na ya nyuma, lakini hutajwa mara nyingi kwa mafungamano na tupu ya mbele..................................




Post a Comment

No comments