Fadhila Za Kutembelea Mgonjwa, Kumlisha Aliye Na Njaa Na Kunywesha Aliye Na Kiu
عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ:
يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي، قَالَ:
يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا
عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ
أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ؟ يَا ابْنَ آدَمَ،
اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي ، قَالَ: يَا رَبِّ وَكَيْفَ
أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ
اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ
لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟ يَا ابْنَ آدَمَ
اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ
وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ
تَسْقِهِ، أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟)) مسلم
Kutoka Kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ((Hakika Allaah ‘Aliyetukuka na Jalali Atasema
siku ya Qiyaamah: Ee mwana wa Adam, Niliumwa na usije kunitembelea?
Atasema: Ee Rabb (Mola), vipi nije kukutembelea nawe ni Rabb wa
ulimwengu? Atasema: Kwani ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa
na hukwenda kumtembelea! Hukujua kuwa ungekwenda ungalinikuta Niko
pamoja naye? Ee mwana wa Adam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema:
Ee Rabb, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema:
Kwani hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa?
Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ee
mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi
nitakupa maji na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Mja wangu fulani
alikuomba maji na hukumpa. Hukujua kwamba ungalimpa maji ungalikuta hayo
(jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]
No comments