Header Ads

Cup of coffee on saucer

MWENYE KWENDA KWA MGANGA AYAJUEE HAYA KWANZA



عَنْ صَفِيَّةَ بِنْتِ أبِي عُبِيْدٍ عَنْ بَعْضِ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَ (رضي الله عنهم) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلاَةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً)) مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Swafiyyah bint Abi ‘Ubayd kutoka kwa baadhi ya wakeze Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mwenye kumwendea mtazamiaji [mpiga ramli] akamwuliza jambo na akamsadiki, hatokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)).[1]

Mafunzo Na Hidaaya:

  1. Haramisho la kuwaendea watabiri na makahini na kusadiki wayasemayo na kwamba Swalaah haitokubaliwa siku arubaini.

  1. Kuna hatari kubwa ya kumsikiliza mtabiri au kahini na kumwamini, kwani kutamkosesha Muislamu thawabu za ‘amali njema kama Swalaah, kwani hiyo ni aina ya shirki kwa vile anaingilia elimu ya ghayb ya Allaah (سبحانه وتعالى) na hivyo hukutoka mtu nje ya Uislamu [Hadiyth: ((Mwenye kumuingia mwenye hedhi, au mwanamke kwa nyuma, au kumwendea mchawi na kumuamini kwa anayosema, basi amekufuru aliyoteremshiwa Muhammad)).[2]

  1. Umuhimu wa kujifunza mas-alah ya hatari kama haya ambayo humtoa mtu katika Uislamu. Ni kwa kuwa, masuala haya ni dhambi Asizozisamehe Allaah (سبحانه وتعالى). [An-Nisaa 4: 48, 116],  na kwamba anayemshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) ataharamishwa na Pepo, bali pia makazi yake yatakuwa ni ya motoni!

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٧٢﴾


Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”[3]

Pia [Rejea Hadiyth namba 108, 136].

  1. Wayasemayo watabiri yanayotokea kweli ni kwa kuwa wamepatiwa habari kutoka kwa majini wanaotega sikio, kisha kuyahamisha kwa wengine. [Al-Jinn 72: 6-10].

  1. Ieleweke kuwa mbali na kutokubaliwa Swalaah siku arubaini, Muislamu aliyefanya kosa hilo ni lazima aswali. Kutoswali kwake ni dhambi nyingine kubwa.

No comments