Sura Ya Sitini Na Tisa: al-Haqqah
Aya 1 – 18: Tukio La Haki Ni Nini Tuko La Haki
Maana
Tukio la haki. Nini hilo Tukio la haki?
Makusudio ya tukio la haki ni Kiyama. Kimeitwa hivyo kwa sababu ni wajibu kutokea kwake. Ama kuuliza na kukaririka, ni kwa ajili ya kuhofisha ukali wake na vituko vyake; kwamba ni tukio ambalo masikio hayajawahi kusikia, macho hayajapata kuona wala akili haijawahi kuwazia. Ndio maana Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akalirudia swali kwa kusema: Na nini kitakujulisha nini hilo Tukio la haki?
Thamudi na A’di walikadhibisha tukio linalogonga.
Thamud ni watu wa Swaleh na A’d ni watu wa Hud. Tukio linalogonga ni katika majina ya Kiyama, kama tukio la haki.
Basi Thamudi waliangamizwa kwa tukio kubwa mno, ambalo ni ukelele wa adhabu. Umeitwa hivyo kwa sababu ya ukali wake.
Na ama A’di waliangamizwa kwa upepo mkali wenye nguvu, wenye kuangamiza.
Aliowapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo.
Upepo uliendelea kwa muda huo bila ya kusita.
Utaona watu wamepinduka ardhini kama kwamba ni magogo ya mitende yalio wazi ndani.
KWA KUSIKILIZA DARSA HII NA KUIHIFADHI NDANI YA SIMU AU KOMPYUTA YAKO BONYEZA HAPA
No comments