Dunia yalaani shambulizi la kigaidi la New Zealand
Viongozi mbalimbali duniani wametuma salamu za rambi rambi zilizoambatana na kulaani kwa nguvu shambulizi la kigaidi dhidi ya misikiti miwili lililopelekea vifo vya watu 49 nchini New Zealand
Dunia nzima imelaani kwa nguvu shambulizi la silaha lililotokea katika misikiti miwili kijiji cha Christchurchnchini New Zealand lililopelekea vifo vya watu 49.
Taarifa ya maandishi iliyotolewa na mwakilishi mkuu wa mahusiano ya kimataifa na sera za ulinzi wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini inasema kwamba,
Wanatoa pole kwa wafiwa wote waliopoteza ndugu na jamaa zao katika shambulizi la kigaidi la New Zealand. Na kwamba mashambulizi katika nyumba za ibada yanahesabika ni mashambulizi dhidi ya watu wote.
Naye rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk kwa kutumia mtandao wa Twitter ametuma ujumbe usemao, Shambulizi la kihaini la Chistchurch haliwezi kuathiri uvumilivu na ustaarabu wa New Zealand
Huku rais wa bunge ala Ulaya Antonia Tajani alisema,
Picha za shambulizi la New Zealand zimeacha watu midomo wazi, ubaguzi wa rangi, chuki na ukichaa ndio vinaweza kumfanya mtu akawashambulia watu waliokuwa kwenye ibada msikitini.
Naye katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ametuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter unaolaani shambulizi hilo la kigaidi dhidi ya misikiti miwili.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma ujumbe wa salamu za pole kwa rais wa New Zealand.
Katika ujumbe huo Putin amesema,
“Shambulizi dhidi ya raia waliokuwa kwenye ibada, ni kitendo kinachotengeneza chuki na kuleta mshangao, natumaini kila anayehusika na tukio hilo ataadhibiwa kadiri inavyostahiki”.
Rais wa Urusi alituma pole kwa wafiwa wote na kuwatakia majeruhi wapone haraka.
Naye msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa jamii kwa niaba ya kansela wa Ujerumani bi Angela Merkel amesema.
Inahuzunisha kitendo cha watu waliokuwa wakifanya ibada yao kwa amani kushambuliwa na kuuawa, tunapinga kwa nguvu zote aina hii ya ugaidi.
Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas kupitia ukurasa wa Twitter alisema wapo pamoja na wahanga wa shambulizi la kigaidi la New Zealand.
Maas aliandika,
"Kitendo cha shambulizi la kigaidi dhidi ya waislamu waliokuwa kwenye ibada, wakiswali kwa amani ni cha kinyama. Kama binadamu ameuawa kwa ajili tu ya dini yake basi shambulizi hili ni dhidi yetu sote. Sisi tupo pamoja na waliopoteza maisha”
No comments