Header Ads

Cup of coffee on saucer

JE MAJI YANATOSHELEZA KUWA DAKU?

🕋 *Maji Yanatosheleza Kama Daku?*🕋

*Swali:* _Kuna watu wanachukulia usahali wa daku pale ambapo wanalala saa 03:00 ya usiku na wanasema kuwa wataamka kabla ya Fajr na kunywa maji na kwamba hilo linatosheleza. Unasemaje juu ya hilo?_

*Jibu:* Ndio, ni kweli ya kwamba inatosheleza. Lau mtu atakula daku katikati ya usiku na kisha akaamka kabla ya kuingia Fajr na kunywa kitu inatosheleza. Hili halina shaka yoyote. Lakini bora zaidi ni kuchelewesha daku mwisho wa usiku. Huu ndio uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imesimuliwa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

*"Watu hawatoacha kuwa katika kheri maadamu ni wenye kuharakisha kukata swawm na kuchelewesha daku."*

Kuhusiana na sentesi ya kwanza:
Watu hawatoacha kuwa katika kheri maadamu ni wenye kuharakisha kukata swawm... "
imethibiti katika "as-Swahiyh" ya al-Bukhaariy na Muslim.

Ama ya pili:
"... na kuchelewesha daku."

imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata kama itakuwa haikusihi kuwa ni maneno yake imesihi katika vitendo vyake. Alikuwa alichelewesha kula daku.

🌴 *Mzungumzaji: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn*🌴

🌷 *Chanzo: Liqaa-aat Ramadhwaaniyyah 1410 H (01 B)*🌷

No comments