MAINGILIANO KATI YA MKE NA MUME
*Fatwa za Mstahiwa Sheikh Ahmed Al Khaliliy.*
(Muft Mkuu wa Oman.)
_Mfasiri: Sheikh Munir Al Masroury._
*MAINGILIANO YANAYOHUSIANA MKE NA MUME.*
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
*SUALI;*
Nini kauli ya Sharia kuhusu mke kunyonya uume wa mumewe wakati wa kuingiliana?
*JAWABU;*
Kunyonya uume kunaweza kuwa ni kunyonya najsi. Hilo ni kwasababu kufikiria kuingiliana hupelekea kutokwa madhii, achilia mbali kushikana mwili na kujitayarisha kwa ajili ya kuingiliana. Madhii ni najsi, na mdomo ni sehemu ya kumtaja Allah na ya kulia fadhila zake katika vyakula na vinywaji; na kwa hiyo haijuzu kwa mwanamke kunyonya uume wa mumewe, kama ambavyo haijuzu kwa mwanamme kuramba utupu wa mkewe; yote hayo ni kwa ajili ya kujitahidi kuepuka najsi-
*إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ.*
*Hakika Allah huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa.*
*Na Allah anajua zaidi.*
➖➖➖➖➖➖➖➖➖

No comments