Header Ads

Cup of coffee on saucer

NI IPI HUKMU YA KUZIKA MAITI MSKITINI ?


97. Ni ipi hukumu ya kuwazika maiti misikitini?
Swali: Ni ipi hukumu ya kuwazika maiti misikitini?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuwazika maiti
misikitini na amekataza makaburi yasifanywe ni mahala pa kuswalia na
amemlaani yule mwenye kufanya hivo wakati alipokuwa katika hali ya
kukata roho. Ameeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni
katika matendo ya mayahudi na manaswara162. Aidha kitendo kama hicho
kinapelekea katika shirki. Kuyafanya makaburi ni mahala pa kuswalia na
kuwazika maiti ndani ya misikiti kunapelekea katika shirki kwa kuwa watu
wanaweza kufikiria kuwa hawa waliozikwa wana uwezo wa kunufaisha na
kudhuru na wana sifa maalum ambazo zinapelekea kushirikishwa pamoja na
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni wajibu kwa waislamu watahadhari
kutokamana na madhihirisho haya ya khatari na wahakikishe misikiti haina
kaburi kabisa na ijengwe juu ya Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi. Allaah (Ta´ala)
amesema:
"Hakika sehemu zote za kuswalia ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe
yeyote pamoja na Allaah."
163
Ni wajibu misikiti iwe kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na iwe
imetakasika kutokamana na madhihirisho haya ya shirki yanayosababisha
kuabudiwa wengine badala ya Allaah. Huu ndio wajibu wa waislamu164.
98. Kuacha wasia wa kuzikwa msikitini 
Swali: Kuna mtu alijenga msikiti na akaacha anausia azikwe ndani yake na 
akazikwa. Kufanywe nini sasa?
Jibu: Wasia huu sio sahihi. Misikiti sio makaburini. Haijuzu kuzika msikitini. 
Ni haramu kutekeleza wasia huu. Lililo la wajibu sasa ni kulichimbua kaburi 
hili na kulizika kwenye makaburi ya waislamu165.


No comments