Mahakama nchini India imeamuru
polisi nchini humo kufanya uchunguzi kwa familia ya Mohammed Akhlaq
inayodaiwa kuchinja ng'ombe kwa makusudi.Mwaka uliopita Akhlaq ambaye ni muislamu anayetokea kijiji kilicho karibu na Delhi,aliuawa kwa tuhuma za familia yake kuhifadhi na kutumia nyama ya ng'ombe nyumbani kwao.
Baba wa mmoja wa vijana wanaotuhumiwa kumuua Akhlaq,anasema familia yake inapaswa kuchunguzwa kwakuwa kuna vielelezo vya kutosha kuwa nyama iliyokutwa ilikuwa ya ng'ombe.
Kesi hiyo imesababisha kuenea kwa hasira na mjadala mkali kuhusu uvumilivu wa kidini nchini humo.
Wahindu wanaamini kuwa ng'ombe ni mtakatifu na kwa wengi, kula nyama yake ni mwiko.
Ng'ombe kuchinjwa ni marufuku sehemu kubwa ya nchi ya India.
No comments