
Je, hii ni kweli? na kama ni kweli naomba nifahamishe uzuri pamoja na hiyo dua manake sikuifahamu uzuri kuiandika siku niliyoisikia kwenye radio.
Shukran.
JIBU:
Sifa
zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani
zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mas-ala ya du’aa. Hakika ni kuwa
Hadiyth hiyo uliyoitaja ni sahihi kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) alisema:
“Rakaa mbili kabla ya Alfajiri ni bora kuliko dunia na viliyomo ndani yake” (Muslim na at-Tirmidhiy kutoka kwa ‘Aaishah [Radhiya Allaahu ‘anha]).
Kwa fadhila na ubora huo ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuziacha daima (al-Bukhaariy).
Ibn
al-Qayyim anatueleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) alikuwa akiziswali akiwa mjini au katika safari.
Ama kuhusu kisomo ni kama ulivyosikia mbali na kwamba vipo visomo vyengine kama tutakavyoeleza. Visomo sahihi ni kama vifutavyo:
- Katika rakaa ya kwanza utasoma Suratul-Faatihah na al-Kaafiruun na ya pili al-Faatihah na al-Ikhlaasw (Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah [Radhiya Allaahu ‘anhu]).
- Hadiyth nyingine inatufahamisha: Rakaa ya kwanza utasoma al-Faatihah na ayah ya 136 ya Suratul-Baqarah na rakaa ya pili al-Faatihah na ayah ya 64 ya Surat al-‘Imraan (Muslim na an-Nasaa’iy kutoka kwa Ibn ‘Abbaas [Radhiya Allaahu ‘anhuma]).
- Au pia katika rakaa ya pili akasoma baada ya al-Faatihah, ayah ya 52 ya Surat al-‘Imraan (Muslim na Abu Daawuud kutoka kwa Ibn ‘Abbaas [Radhiya Allaahu ‘anhuma]).
Ama
kuhusu du’aa hiyo uliyotaja zipo Hadiyth nyingi zinazozungumzia kuwa
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma ima
baada ya Swalah, au usiku anapoamka kwa Tahajjud au katika Sunnah ya
alfajiri bila kusema ni katika rakaa ya ngapi, au katika Qunuut ya
Swalah ya Witri lakini zote ni dhaifu. Ama ile iliyopatikana katika
sijdah ya rakaa ya mwisho ilisomwa na Swahaba aliyeshikwa na jambazi na
akaomba aruhusiwe kuswali Swalah kabla ya kuuliwa. Aliruhusiwa naye
akaswali sunnah ya rakaa nne na katika sijdah ya mwisho akawa ni mwenye
kusoma du’aa ndefu kikiwemo kifungu hiki lakini hii ni Mawdhuu‘ (ya kutungwa/ kubuni kama anavyosema Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn al-Albaaniy).
Hakika
ni kuwa du’aa za kusoma ukiwa katika sijdah zipo nyingi ambazo zinaweza
kusomwa katika Swalah yoyote ile – iwe ni ya faradhi au ya Sunnah
katika rakaa ya kwanza au ya pili na hiyo uliyoitaja si miongoni mwazo.
Hivyo ni bora kutumia zile zilizosuniwa kuliko kutumia hiyo ila
papatikanwe mapokezi yaliyo sahihi kuhusu hilo.
No comments