SWALI:
Assalam allaykum warahmatullahi
Kwanza napenda kuwapongeza wote wanaoshiriki katika kazi hii ya kuelimisha umma wa kiislam hasa kwa sisi ambao tuko kwenye nchi hizi za kimagharibi . Ahsanteni sana na allah atawajaza majazo mema leo duniani na kesho akhera. Suali langu ni hili tokea kukaribia kumi la mwisho la mwezi huu mtukufu wa ramadhan nimekuwa napokea email kutoka watu mbali mbali zinazoelezea kuhusu sala ya laylatul Qadri ambayo husaliwa kwa rakaa zaidi ya kumi na moja pamoja sura zake maalum kwa kila siku (yaani kila siku na sura zake maalum) kwa mfano kuna siku usome sura zinazoanza na haa mim na nyenginezo pia ikiwemo salatul tasbihi. hivyo naomba nasaha zenu watu wa alhidaaya kwani tumo ndani utata mkubwa waislam. Assalam alaykum warahmatullhi
Kwanza napenda kuwapongeza wote wanaoshiriki katika kazi hii ya kuelimisha umma wa kiislam hasa kwa sisi ambao tuko kwenye nchi hizi za kimagharibi . Ahsanteni sana na allah atawajaza majazo mema leo duniani na kesho akhera. Suali langu ni hili tokea kukaribia kumi la mwisho la mwezi huu mtukufu wa ramadhan nimekuwa napokea email kutoka watu mbali mbali zinazoelezea kuhusu sala ya laylatul Qadri ambayo husaliwa kwa rakaa zaidi ya kumi na moja pamoja sura zake maalum kwa kila siku (yaani kila siku na sura zake maalum) kwa mfano kuna siku usome sura zinazoanza na haa mim na nyenginezo pia ikiwemo salatul tasbihi. hivyo naomba nasaha zenu watu wa alhidaaya kwani tumo ndani utata mkubwa waislam. Assalam alaykum warahmatullhi
Barua yenyewe ni hii:
ASSALAM ALAYKUM,
NDUGU ZANGU WAISLAM NAWAOMBA TUFANYE BIDII NA JITIHADA NA KUHAKIKISHA
KILA MMOJA WETU ANATEKELEZA SALA HII PINDI HALI IKIMRUHUSU, INSHAALLAH.
TAREHE 21 USIKU - MWEZI WA RAMADHANI NDUGU ZANGU WAISLAM NAWAOMBA TUFANYE BIDII NA JITIHADA NA KUHAKIKISHA
KILA MMOJA WETU ANATEKELEZA SALA HII PINDI HALI IKIMRUHUSU, INSHAALLAH.
a) USIKU WA TAREHE 21 SALI RAKAA 4, TOA SALAM KILA BAADA YA RAKAA 2. KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1, AL-QADIR x 1 NA IKHLAS x 1 UKIMALIZA MSALIE MTUME (S.A.W) x 70.
b) USIKU HUO HUO - SALI RAKAA 2, KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1,
AL-QADIR x 1 NA IKHLAS x 3. BAADA YA SALAM VUTA URADI
UFUATAO:
"ASTAGHGIRULLAHI LLADHI LAILAHA ILLA HUWA
WAATUBU ILAYHI" x 70.
c) VILE VILE USIKU HUO HUO WA TAREHE 21 SOMA SURAT QADR x 21.
USIKU WA TAREHE 23 - MWEZI WA RAMADHANI
a) SALI RAKAA 4(MBILI MBILI), KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1,
AL-QADIR x 1 NA IKHLAS x 1. BAADA YA SALAM MSALIE MTUME (S.A.W) x 70.
b) USIKU HUO HUO - SALI RAKAA 8 (MBILI MBILI), KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1, AL- QADIR x 1 NA IKHLAS x 1. UKIMALIZA VUTA URADI UFUATAO:
"SUB-HANA LLAHA WALHAMDULLILLAHI WALAILAHA ILLALLAHU WALLAHU AKBARU" x 70.
c) VILE VILE USIKU HUO HUO WA TAREHE 21 SOMA SURAT YASEEN x 1 NA ARRAHMAN x 1.
USIKU WA TAREHE 25 - MWEZI WA RAMADHANI
a) SALI RAKAA 4 (MBILI MBILI), KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1,
AL-QADIR x 3 NA IKHLAS x 3. BAADA YA SALAM LETE ISTIGHFARA
"ASTAGHFIRULLAHI LLADHI LAILAHA ILLA HUWA WAATUBU ILAYHI" x 70.
(Sala hii ni nzuri kwa kusamehewa dhambi zako).
b) USIKU HUO HUO - SALI RAKAA 2, KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1,
AL- QADIR x 1 NA IKHLAS x 15. UKIMALIZA SOMA "LAILAHA ILLALLAH MUHAMMAD RASULULLAH"
c) VILE VILE USIKU HUO HUO WA TAREHE 25 SOMA SURAT DUKHAN x 7
UNAEPUSHWA NA ADHABU YA KABURINI. VILE VILE SOMA SURAT FAT-HA x 7.
USIKU WA TAREHE 27 - MWEZI WA RAMADHANI
a) SALI RAKAA 4 (MBILI MBILI), KILA RAKAA SOMA SURAT FAT-HA x 1,
AL-QADIR x 3 NA IKHLAS x 50. BAADA YA KUTOA SALAM SUJUDU NA USOME:
SUB-HANA LLAHA WALHAMDULLILLAHI WALAILAHA ILLALLAHU WALLAHU AKBARU.
Kisha omba haja zako kwa Mola wako (yeye ndie mtoaji).
b) USIKU HUO HUO SOMA SURA SABA (7) ZENYE KUANZA NA "HAAMMIIM". PIA
SOMA SURAT "MULK"x 7.
SALAT TAS-BIHI.
VIZURI KUSALIWA MWEZI WA RAMADHAN NA HASA TAREHE 26.
KUMI LA MWISHO LA RAMADHAN:
a) KILA SIKU SOMA "LAILAHA ILLA-LLAH SADIQAN LAILATUL QADR".
b) VILE VILE KATIKA KUMI HILI KILA SIKU BAADA YA SALA YA ISHAA SOMA
SURAT
QADR x 7.
IJUMAA LA MWISHO WA MWEZI WA RAMADHANI KABLA YA SALA YA ADHUHURI SOMA
SURAT QADR x 3.
1. BAADA YA SALA YA ADHUHURI/IJUMAA SALI RAKAA 2:
RAKAA YA KWANZA SOMA SURAT FAT-HA x 1, IKHLAS x 10,
ZULZILAT x 1.
RAKAA YA PILI SOMA SURAT FAT-HA x 1, ALKAFIRUN x 3. BAADA YA SALAM
MSALIE MTUME (SAW) x 10, BAADAE
2. SALI RAKAA 2 NYENGINE:
RAKAA YA KWANZA SOMA SURAT FAT-HA x 1, TAKATHUR x 1, IKHLAS x 10.
RAKAA YA PILI SOMA SURAT FAT-HA x 1, AYATUL KURSIYYU x 3, IKHLAS x 25
(Thawabu za sala hii zinaendelea
mpaka siku ya kiama).
NDUGU MUISLAM, TUPATE NINI TENA KUTOKA KWA MOLA WETU, KILA YA NJIA YA KUJJIPATIA MEMA AMETUWEKEA.
MTUMIE NA MUISLAM MWENZIO IKIWA NI MWENYE KUAMINI NA MWENYE IMANI YA
KWELI.WAALAYKUM SSALAAM.
JIBU:
Sifa
zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,
Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)
na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakika
ndugu Waislamu, kutokana na utamaduni wa mawasiliano siku hizi kwa
kupatikana njia nyingi za kutuma ujumbe kupitia barua pepe (e-mail) au
katika simu za mkono (text messages) n.k, uzushi mwingi umekuwa
unarushwa na kuwafikia Waislamu wengi ambao nao bila ya kujua wanapata
mafunzo yasiyo sahihi, nao wanawatumia wenzao, hivyo hivyo inaendelea
hadi kuwafikia maelfu wa Waislamu.
Yafutayo ni maelezo tunayowatahadhirsha ndugu zetu wote kuhusu ujumbe huu:
- Si Hadiyth ya MTUME (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).bali ni maneno yaliyopangwa na baadhi ya watu kuwashughulisha tu Waislam wakaacha kufanya yale yaliyo SAHIHI na YALIYOTHIBITI kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
- Ibada yoyote ile kwa mpangilio wa idadi na namba, inahitaji ushahidi na dalili. Zikikosekana basi inatupasa kuziacha na kutozifanyia kazi.
- Barua kama hizi zinazorushwa hakika zinawashughulisha sana Waislam na wengi wakihadaika wakidhani ni mambo ya Dini na hali ni mambo yasiyokuwepo na yaliyotungwa tu na watu.
- Hii pia inawasababishia pia Waislam kukosa kheri na fadhila za kufanya ibada zilizothibiti zenye dalili ambazo zingewaongezea ujira mkubwa haswa katika masiku haya matukufu ambayo tumesisitizwa sana kuongeza juhudi katika ibada.
Tunatoa
nasaha kwa ndugu zetu katika Iymaan musiwe na haraka ya kueneza mambo
ambayo yanadhaniwa ni Hadiyth au mafunzo ya Dini na hali ni utungo tu
kutoka kwa wasio na kazi ila kuwashughulisha watu na kuwapotezea muda
wao kwa mambo ambayo hayawezi kuwapatia ujira bali watarudishiwa wao na
kutopata kitu zaidi ya kupoteza muda. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) kapinga hilo sana na kalikemea vikali pale aliposema:
(Mwenye Kuzusha jambo katika DINI yetu hii, basi litarejeshwa kwake) [Al-Bukhaariy na Muslim]. Yaani hatopata kitu zaidi ya kuua muda wake na kujichosha bure!
Tujihadhari
na barua nyingi tuzipatazo kwenye internet kwani nyingi huwa ni mambo
ya uongo na kutungwa na pia kusingiziwa nayo Dini na Mtume (Swalla
Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ametuonya kwa maonyo makali kama haya:
((من كذب علي متعمدا فليتبوأ مقعده من النار)) متفق عليه
((Atakayeniongopea makusudi basi ajitayarishie makazi yake motoni)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Tunawaomba
ndugu zetu msome makala MUHIMU zifuatazo ambazo zina maelezo mengi
kuhusu hatari ya kusambaza uzushi, ili kila mmoja wetu ajiepushe na uovu
huo:
No comments