Header Ads

Cup of coffee on saucer

MKENYA ANYAKUA GARI KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURANI JIJINI DAR ES SALAAM

Mohamed Moge Aden mwanafunzi kutoka nchini kenya amefanikiwa kuwa mshindi wa juzuu Thelathini katika mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qurani yaliyofanyika leo Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yaliyoshirikisha wanafunzi kutoka nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda na Uganda yaliandaliwa na Taasisi ya Alhikma Education Centre inayoongozwa na Sheikh Abdulqadir Al ahdar.

Mashindano hayo yaliyohudhuriwa na maelfu ya waislamu, Juzuu zilizoshindaniwa ni kuanzia juzuu moja, tatu, tano, saba, kumi, ishirini na thelathini.

Mshindi huyo wa kwanza amepata zawadi ya gari aina ya Noah yenye thamani ya shilingi milioni kumi na tatu.

Zawadi hii ya gari kwa mshindi wa kwanza ni kubwa kuliko zote zilizowahi kutolewa katika mashindano ya kuhifadhi Qurani kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati.

Mshindi wa pili wa juzuu 30 ni kutoka Tanzania Rajab Juma Mdomondo aliyepata Min Ipad na Dola 3000. Mshindi wa tatu Uwimana Yusuf Juma kutoka Burundi amepata Min Ipad na dola 2000.

Washindi wa juzuu 20 ni Juzuu 20: 
Mshindi wa tatu ni Suleiman Ramadhani Suleiman, amepata baiskeli na Pesa taslimu shilingi 800,000/. 
Mshindi wa pili ni Hamza Khalid Muhammad, amepata Laptop na pesa taslimu shilingi 1,000,000/.
Mshindi wa kwanza ni Abdulbasit Lubeya, amepata pikipiki, na pesa taslimu 1,200,000/.

Washindi wa juzuu 10:
Mshindi wa tatu ni Salumu Hemedi ali, amepata baiskeli na pesa taslimu shilingi 600,000/ Mshindi wa pili ni Hashim Abdulqadir, amepata Laptop na pesa Taslimu shilingi 800,000/.
Mshindi wa kwanza ni Ahmed Muhammad Ali, amepata pikipiki na pesa taslimu shilingi 1,000,000.

Washindi wa Juzuu 7:
Mshindi wa tatu ni Ramadhani hussein miaka 6, amepata radio subwofer na pesa taslimu Shilingi 500,000/.
Mshindi wa pili ni Hussein said kibari, amepata Radio subwofer na pesa taslimu shilingi  700,000/.
Mshindi wa kwanza ni Twalha Hamoud Masoud, amepata friji kubwa na pesa taslimu shilingi  900,000/.

Washindi wa Juzuu 5:
Mshindi wa tatu ni Salma Mohamed Masoud, amepata cherehani na pesa taslimu shilingi 300,000/.
Mshindi wa pili ni  Sakina Ashraf Halfan amepata Cherehani na pesa taslimu shilingi 500,000/.
Mshindi wa kwanza ni Salim Arif Abdallah, amepata friji ndogo na pesa taslimu shilingi 700,000/.

Washindi wa Juzuu 3:
Mshindi wa tano ni Halifa Hamis Saleh amepata birika ya kuchemshia maji na pesa taslimu shilingi 200,000/.
Mshindi wa nne ni Siraji Hassan amepata birika ya kuchemshia maji na pesa taslimu shilingi 250,000/.
Mshindi wa  tatu ni Sudais Suleiman kirungi, amepata radio subwofer na pesa taslimu shilingi 300,000/.
Mshindi wa pili ni Khuzeima Ramadhani amepata Cherehani na pesa taslimu shilingi 400,000/.
Mshindi wa kwanza ni Muhiya Omar Muhiya amepata TV Flat Screen na pesa taslimu shilingi  600,000/.

Washindi Juzuu 1:
Mshindi wa tano ni omar suleiman Liberi, amepata birika ya kuchemshia maji na pesa taslimu shilingi 100,000/.
Mshindi wa nne ni Ahmed Hamisi halfani, amepata birika ya kuchemshia maji na pesa taslimu shilingi 200,000/.
Mshindi wa tatu ni Rehema Faki Ahmad, amepata Rice Cooker na pesa taslimu shilingi 300,000/.
Mshindi wa pili ni Muhibu Hamis Bakari amepata Rice Cooker na pesa taslimu shilingi 400,000/.
Mshindi wa kwanza ni Ahmed muhamed, amepata TV Flat screen na pesa taslimu shilingi 500,000/.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa ni Rais Msataafu Ali Hassani Mwinyi. 

Masheikh wengi walihudhuria akiwemo Kaimu Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zubeir, Kadhi Mkuu Sheikh Abdallah Mnyasi na masheikh kadhaa wa taasisi mbalimbali za dini.

Mdhamini mkuu wa mashindano hayo ni benki ya kiislamu ya AMANA.

Post a Comment

No comments