Header Ads

Cup of coffee on saucer

Hadiyth Kuhusu Kuomba Du’aa Pamoja Baada Ya Swalah Ni Swahiyh Au Dhaifu?

Assalam alaikum



Dua after Salah – Dua & AzkarIpo hadithi ya mtume swalla llah alaih wa sallam, ambayo imesimuliwa na Abuu Umama radhiya llah anhu amabyo ni hii hapa. Asema Mtume Swallalhu alai wasallama" hai mwao na wengine wakaitikia aamiin; illikusanyiki kundi la watu; wakaomba dua miongona allah atawajibu" amepokea Twabrani, Baihaqiy, Hakim kutoka kwa Habibi Ibn Salamatal Fihryyah; Allah awa wee radhi wote hao.

Hii ndio hadithi ninayotaka kujuwa usahihi wake na kama ni sahihi ukiunganisha na ya Abuu Umama itakuwa ni shaihi kuomba dua kwa pamoja baada ya swala ya fardhi? Kwani imethibiti dua ya pamoja na pia imethibiti dua baada ya swala. Yaani moja ya sehemu inayo kubalika dua ni baada ya swala ya faradh na kama alivyosema imamu Tirmidhy (Allah amrehemu) kuwa ni hadithi hasan. Je? hadithi hii inafaa kuwa ni hoja madhubuti kwamba kuomba dua baada ya swala ya fardh ni sunnah na imethibiti kwa mtume Swalla llah alaih wa sallam na ni muhimu sana kwa mtu kuomba dua baada ya swala ya fardhi kwani ni moja ya sehemu inayokubaliwa dua



MAELEZO MENGINE YA MUULIZAJI KUHUSIANA NA SWALI LAKE



Assalam alaikum,

Hadithi ya Abuu Umama niloisema yazungumzia dua baada ya swala ni hii hapa kama alivyo inukuu Imamu Shaukani ktk Nailu L’autwar. Pia hadithi hii inapatikana ktk Riyadha swallihina hadithi ya 1,500. Pia nime attach hadithi nilo andika kwa mkono, hii nimeikuta ktk vitabu hivi vya dua vidovidogo, sijaiona ktk vitabu vya hadithi, nimeikopi pamoja na muhtasari wa takhrij yake,sina hakika na usahihi wa hadithi hii



1.     Swali la kwanza, naomba mnifahamishwe usahihi wa hadithi nilo andika kwa mkono (attachment number one) ama umadhubuti wake kama inafaa kufanyia kazi

2.     Maelezo kwa ufupi: Hadithi ya Abuu Umama; Ibn Hajar ktk Fathu lbar juzu ya 11 ukurasa 153 (toleo la mwaka 2003) Kitabu dda’awa (dua’u ba’ada swalat)  ameinukuu na akaunganisha na hadithi ya Twabari kutoka kwa jaafar isemayo” dua baada ya swala ya Fardh ni bora kuliko dua baada ya swala ya sunnat kama ilivyo kuwa ubora wa swala ya fardh kwa swala ya sunnat” pia akanukuu manenoya Watu wa Hanbal kuhusu kauli ya Ibn Lqaiym ktk kitabu chake cha Zadu l’ma’aad (alipo sema hakuna hadithi sahihi inayo thibitisha  dua baada ya swala)

3.     Swali la pili, Ikiwa hadithi ya Abuu Umama na maelezo ya Ibn Hajar na hadith ya Twabari ni sahihi; Je kuomba dua baada ya swala ya Fardh ni Sunnat?

4.     Swali la tatu, ikiwa hadithi nilo andika kwa mkono (Swali la kwanza) ni sahihi ama ni madhubuti na inafaa kufanyia kazi, na kwa kuwa baada ya swala kuna kundi la watu, hivyo wakaamuwa miongoni mwao mmoja aombe dua na wengine waitikie wakaifanyia kazi hadithi (kwani ni sababu ya kujibiwa dua kama haidthi inavyo jieleza) na kwa kuwa kuomba dua baada ya swala ni sahihi ikiwa Swali la pili  yaani hadithi ya Abuu Umama  ni madhubuti, Je, kuomba dua kwa pamoja baada ya swala( yaani kufanyia kazi hadithi nilo andika kwa mkono na ya Abuu Umama kwa pamoja) itakuwa ni sunnat ama bid’a( ukizingatia sunnah inaweza kuwa Mtume Swalla llahu alaihi wa sallam amesema(sio lazima afanye), ama amefanya, amekubali jambo moja ktk ya haya matatu yaweza kuwa sunnat)



Wabillah taufiq
 

No comments