Abubakar Shekau, kiongozi wa wanamgambo wa Boko haramu Nijeria amejitokeza na kukana uvumi kuwa alikuwa ameuawa.
Madai ya kufariki kwa Shekau yalianzishwa na raisi wa Chad Idriss Deby.
Shekau alijirikodi na kusambaza katika vyombo vya habari.
Idara
ya upelelezi nchini Nijeria yenye utaalamu ilichunguza rikodi ya
Shekau na wakathibitisha kwamba sauti hiyo bila shaka ilikuwa ya
Shekau.
Mwaka
2014 raisi wa Chad alikuwa akikutana na wanamgambo wa Boko haram kwa
lengo la kuleta amani baina yao na serikali ya Nijeria.
Majuma mawili yaliopita, serikali ya Chad ilidai kuwaua wanamgambo 117 wa Boko haram katika visiwa vya ziwa la Chad.
Boko haramu wamewaua zaidi ya watu 600 nchini Nijeria chini ya uongozi wa raisi Muhammadu Buhari.

No comments